Tuesday, January 27, 2009

DJ CHOKA APATA AJALI.........


Dj wa Muziki wa Hiphop na kundi la Chokombaya Dj choka alipata ajali mbaya iliyotokea katika maeneo ya Upanga. Hugoline Martin aka Dj Choka akiwa na gari ya Prof Jay aina ya Benz Black,alipata ajali hiyo ijumaa kuamkia jumamosi akitokea kununua Luku maeneo ya Fire na kurudi na barabara ya Umoja wa mataifa ndipo tairi la kushoto la mbele la gari hiyo lilipopata pancha kwenye njia panda ya kwenda Muhimbili na Diamond Jubilee na hatimaye kuyumba , kutokana na jitiada zake hakumgonga mtu yoyote wala hakugonga gari la mtu. Gari hilo lilienda kugonga ukuta wa nyumba ya jirani na barabara ya Umoja wa mataifa na kazi ikaishia hapo hapo. Hakupata madhara yoyote yale. Glob ya worldhiphop123 inampa pole sana.