Monday, January 12, 2009

Mamluki wanashusha Hiiphop!

Msanii Kulwa Felician Pongo a.k.a BLAC ambaye muziki wake umetokea kubamba ile kinoma ktk kipindi cha mwaka jana ameibuka na kuwatolea uvivu wasanii wa muziki wa Hiphop nchini.
Blac aliyetamba na nyimbo kama 'Kwa Masela' na 'Sema' ametamka kuwa kuporomoka kwa muziki huo kunatokana na ongezeko la wasanii mamluki wanaotumiwa na baadhi ya mameneja kwa lengo la kujinufaisha. Akiendelea anasema kuwa mabosi hao huwatumia ambao hawana uwezo na kulazimisha mambo, ambayo yamekuwa yakitoa taswira kwa jamii kwamba muziki wa hip hop hauna uelekeo....na kudai kuwa ubaya wa wasanii hao tegemezi umewafanya wenye uwezo na hip hop nchini Tanzania kujikuta wakishawishika kufanya muziki wao kuwa chini kwa kufanya maonyesho ya bei chee. "Taratibu utakuta hata hawa wanaoweza wanashawishika kushiriki maonyesho, ambayo wanalipwa mpaka 20,000 na baada ya muda wanazoea na kusahau misingi ya muziki wa hip hop ambao unataka uvumilivu na utulivu wa hali ya juu huku ukifanya kazi kwa bidii kila kukicha kwa ubunifu zaidi ili kuwahamasisha mashabiki kutokuchoka kupenda muziki wako, anasema Blac. "Muziki mgumu, kama hautakuwa imara hautaweza kufika kokote wala kufanya maamuzi yanayofaa, kwa mimi kufanya onyesho kwa 20,000 haiingii akilini ni aibu kwa msanii hata mashabiki wakisikia umelipwa hivyo watakushusha na hawatathamini hata kazi zako," anasema Blac. Blac, ambaye albamu yake ya "Ramani" inafanyiwa kazi nchini Uingereza anasema jambo ambalo halikuwa kawaida kwa wasanii wa hip hop kuimba kwenye matamasha kwa bei nafuu sasa linafanyika na wasanii wa hip hop wanatumbuiza hadi kwa sh. 20,000 kitendo kinachofanya wasanii wote kuonekana hawafai.