Saturday, January 17, 2009

Hard Blasters 2009!

Kundi la muziki wa Hiphop lililojulikana kama Hardblasters na lililotamba na Albam yake ya Funga Kazi 2000 likijumuisha wasanii watatu ambao ni joseph Haule Prof J. Fanani na Willy katika miaka ya 1999 na 2000 sasa linarudi tena kwenye gemu baada ya ukimya wa Takriban miaka kumi hivi.Wakinukuliwa hivi karibuni wasanii wa kundi hilo Prof. J...pamoja na Willy walisema kuanzia mwaka 2009 wanayo project ya kurekodi Albam ambayo itakuwa ni tishio katika muziki wa kizazi kipya, albam hii inaweza kushangaza watu kwani vile vichwa vitatu yaani Joseph Haule aka (Prof.J.) Terry aka (Fanani) na Willy ambavyo ndiyo vilivyoandika mistari na vina katika wimbo wa Chemsha Bongo uliokuwa katika Albam yetu ya Funga Kazi 2000 vinarudi tena kufanya kazi pamoja kama Hardblasters.

Kama unavyojua kwamba wimbo wa Chemsha bongo kutoka Hardblasters kwa wakati ule ndiyo ulichangia kwa kiasi kikubwa sana kuwashawishi wazazi kuwaruhusu watoto wao kuanza kuimba muziki huu, kwani kwa kipindi hicho ulikuwa ukionekana kama muziki wa wahuni.Prof J. au a.k.a Mr.Red Carpert anasema hivi sasa wako kamili...Terry yuko fiti kabisa willy alikuwa amebanwa na majukumu mengi ya kifamilia na mimi programu yangu inaniruhusu kwakuwa niko kwenye gemu kwa muda wote wa maisha yangu hivyo mkakati wetu uko makini na tumeshaanza kuandika nyimbo za kutosha kwa ajili ya Albam hiyo.Utengezaji wa Albam hiyo utakuwa chini ya Maproducer ambao ni Producer Q. , Ludigo na Dj Choka ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika kumiliki mashine kwenye maonyesho yangu.Wasanii hao walisema wana imani kuwa baada ya miaka kumi....watakuja kisasa zaidi....husasan baada ya mwenzao Prof. J....kuwa anaijua zaidi biashara ya muziki...baada ya kushiriki maonyesho kadhaa ya kimataifa.Mbali ya kutamba na wimbo wa Chemsha Bongo Hardblasters pia ilitamba na nyimbo kama mamsap, Niamini,Nataka niwe na wewe, Chuzi limekubali na nyingine nyingi zilizochengua vijana wanaoupenda zaidi muziki huo.
Baada ya washabiki wa muziki wa Hip hop kuwasubili kwa muda mrefu sasa tuone kama itakuwa kweli au ndio longolongo za kila siku.